

Lugha Nyingine
加强学术期刊主题宣传 推动公众健康科普工作—...
NAIROBI - Kenya imetangaza jana Jumatano kuwa itafanya mikutano na Tanzania mapema Agosti ili kushughulikia wasiwasi juu ya hatua za "kubagua" za ushuru na vizuizi vya kibiashara zilizoanzishwa hivi karibuni, ikiwemo marufuku kwa watu wasio raia kufanya biashara ndogo ndogo nchini Tanzania.
Lee Kinyanjui, Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya, amesema hatua hizo zilizoanzishwa na Tanzania juzi Jumatatu zinatishia mafanikio yaliyopatikana katika mafungamano ya kikanda chini ya mfumokazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Ameeleza wasiwasi juu ya Sheria ya Fedha ya Tanzania ya Mwaka 2025 na marekebisho ya hivi karibuni ya Sheria ya Ushuru (Usimamizi na Ushuru) ya Mwaka 2019, ambayo imeanzisha ushuru mpya na tozo ya maendeleo ya viwanda kwa viwango vya asilimia 10 na 15, mtawalia.
Pia amerejelea Amri ya Utoaji Leseni za Biashara (Marufuku ya Shughuli za Kibiashara kwa Watu Wasio Raia) ya Mwaka 2025, ambayo inazuia watu wasio Watanzania kujihusisha na sekta 15 maalum, zikiwamo za biashara ndogo ndogo na ndogo. Amri hiyo, ambayo inajumuisha adhabu kali kwa ukiukaji, imeanza kutekelezwa mara moja, isipokuwa kwa wamiliki leseni wa sasa.
"Hatua hizi ni kubwa na zinadhoofisha malengo ya kimsingi ya mafungamano ya kiuchumi ya kikanda chini ya Itifaki ya Soko la Pamoja," Kinyanjui amesema, akirejelea dhamira ya EAC ya kuunda soko moja ambalo linahakikisha mzunguko huria wa bidhaa, huduma, mitaji, nguvu kazi, na haki za kuishi na kuanzisha maisha.
"Kenya inataka vizuizi hivi viondolewe na Tanzania irejee kwenye hatua zilizowekwa katika itifaki ya EAC," Kinyanjui amesema.
Kinyanjui ameonya kuwa amri hiyo ya utoaji leseni inaonekana kuharamisha vinginevyo uwekezaji halali wa EAC na huenda itaharibu uchumi wa nchi zote mbili.
"Kwa hiyo ni muhimu, kwa moyo wa EAC, kwamba mazungumzo ya pande mbili yafanyike kutatua masuala haya," amesema, akiongeza kuwa majadiliano zaidi ya pande mbili yamepangwa kushughulikia hatua hizo mpya na masuala mengine ya kibiashara yanayoendelea.
Kwa mujibu wa afisa huyo, EAC ni soko kubwa la mauzo ya nje ya Kenya, ikichukua asilimia 28.1 ya mauzo yake yote ya nje, yaliyokuwa na thamani ya dola za kimarekani takriban bilioni 2.3 mwaka 2024. Tanzania ni mshirika wa pili kwa ukubwa wa kibiashara wa Kenya ndani ya EAC kufuatia Uganda, huku biashara ya pande mbili ikiwa na thamani ya dola za Kimarekani milioni 487 mwaka huu.
Mandhari ya Kipekee ya Karst katika Mkoa wa Guizhou yavutia watalii
Tamasha la kimataifa la densi lafunguliwa katika Mkoa wa Xinjiang, China likiwa na maonyesho 52
Wakulima wa China wawa na pilikapilika za uzalishaji wa kilimo katika kipindi cha Dashu
Maliasili nyingi za chumvi zaongeza mapato ya wanakijiji katika Wilaya ya Gegye, Xizang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma