

Lugha Nyingine
高校毕业生图像采集 新华网浙江频道
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa na Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen, ambao wako nchini China kuhudhuria Mkutano wa 25 wa Wakuu wa China na Umoja wa Ulaya, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 24, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China jana Alhamisi alipokutana na Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EU) Ursula von der Leyen, ambao wako Beijing kuhudhuria Mkutano wa 25 wa wakuu wa China na EU, ametoa wito kwa China na EU kutoa utulivu na uhakika zaidi kwa dunia kupitia uhusiano thabiti na mzuri kati ya China na EU.
Akisema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na EU, na maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, Rais Xi amesema uhusiano kati ya China na EU umefika kwenye hatua nyingine muhimu katika historia.
Katika miaka 50 iliyopita, China na EU zimepata mafanikio makubwa katika mawasiliano na ushirikiano, zikinufaishana na kuleta manufaa kwa dunia nzima, amesema, akiongeza kuwa maelewano muhimu ni kwamba pande hizo mbili zinapaswa kuheshimiana, kutafuta mambo ya pamoja huku zikiweka pembeni tofauti, kushikilia kufungua mlango na ushirikiano, na kutafuta kunufaishana.
"Hizi pia ni kanuni muhimu na mwelekeo sahihi kwa uhusiano kati ya China na EU katika siku za baadaye," Rais Xi amesema, akiongeza kuwa wakikabiliwa na kasi ya mageuzi ya kimataifa ambayo hayajapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita na dunia inayobadilika na yenye misukosuko, viongozi wa China na EU wanapaswa kwa mara nyingine kuonyesha dira na uongozi, na kufanya machaguo sahihi ya kimkakati ambayo yatakidhi matarajio ya watu na kustahimili mtihani wa kihistoria.
Rais Xi amesisitiza umuhimu wa China na EU, zote zikiwa nguvu za kiujenzi kwa ushirikiano wa pande nyingi, uwazi na ushirikiano, katika kuimarisha mawasiliano, kuongeza hali ya kuaminiana na kuzidisha ushirikiano katika hali yenye changamoto na ngumu zaidi ya kimataifa, ili kutoa utulivu na uhakika zaidi kwa dunia kupitia uhusiano thabiti na mzuri kati ya China na EU.
Rais Xi ametoa mapendekezo matatu kwa ajili ya maendeleo ya siku za baadaye ya uhusiano kati ya China na EU.
Kwanza, pande zote mbili zinapaswa kushikilia hali ya kuheshimiana na kuimarisha nafasi ya uhusiano wa kiwenzi kati ya China na EU, pili, pande hizo mbili zinapaswa kushikilia uwazi na ushirikiano, na kudhibiti ipasavyo tofauti na mikwaruzano na tatu, Rais Xi ametoa wito kwa pande hizo mbili kutekeleza ushirikiano wa pande nyingi na kushikilia kanuni na utaratibu wa kimataifa.
Kwa upande wao, viongozi hao wa EU wamesema kuwa China imeibuka kuwa nchi kubwa ya viwanda na teknolojia, ikiondoa mamia ya mamilioni kutoka katika umaskini, wakiongeza kuwa maendeleo ya China yametoa msukumo mkubwa kwa dunia, na EU inaamini kuwa China itafikia maendeleo makubwa zaidi na EU itaunga mkono juhudi hizo.
EU na China ni nguvu kuu duniani, na uhusiano kati ya EU na China ni muhimu sana kwa pande zote mbili na dunia", wamesema, wakiongeza kuwa EU ina dhamira ya kuzidisha kwa kina uhusiano kati ya EU na China, kudhibiti tofauti kwa njia ya kiujenzi, na kufikia matokeo mazuri zaidi katika ushirikiano wa pande mbili ambao ni wenye uwiano, wa kutendeana kwa usawa na wenye kunufaishana.
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa na Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen, ambao wako nchini China kuhudhuria Mkutano wa 25 wa Wakuu wa China na Umoja wa Ulaya, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 24, 2025. (Xinhua/Li Xiang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma